Kikosi chetu leo jioni kimefanya mazoezi ya kwanza kwenye Uwanja wa Hali ya Hewa hapa mkoani Kigoma kujiandaa na mchezo wa fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Yanga utakaofanyika Jumapili Uwanja wa Lake Tanganyika.
Katika mazoezi hayo wachezaji wameonekana wakiwa na morali ili kulishawishi benchi la ufundi liwape nafasi ya kucheza.
Kikosi kimewasili mkoani hapa jana jioni kikiwa na wachezaji 24 ambapo wote wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo huo wa fainali.
Benchi la ufundi limeamua kuja na wachezaji wote ili kupata wigo mpana wa kuchagua kikosi kulingana na ukubwa wa mechi husika.