Simba yafanya mazoezi Sudan kuimalizia hasira Al Merreikh

Kikosi chetu leo kimefanya mazoezi hapa Khartoum, Sudan kwenye uwanja unaomilikiwa na Jeshi la nchi hiyo ili kujiweka tayari kabla ya kuivaa Al Merreikh Jumamosi.

Timu iliwasili leo alfajiri nchini hapa na leo imefanya mazoezi ya kwanza huku wachezaji wote wakiwa ‘fit’ tayari kupambania alama tatu muhimu.

Msemaji wa klabu, Hajji Manara amesema Uongozi uliosafiri na timu unahakikisha kila kitu kinapatikana kwa wakati ili wachezaji wasipate changamoto yoyote kabla ya mtanange huo.

“Kwa sasa Simba imejipanga kushinda katika kila mechi iwe nyumbani au ugenini lakini tunakiri mchezo utakuwa mgumu lakini tumejipanga kuwakabili wapinzani wetu.

“Kikubwa tunahitaji dua na maombi kutoka kwa Wanasimba na Watanzania popote walipo ili kuhakikisha tunapata ushindi,” amesema Manara.

Katika msimamo wa Kundi A, Simba ndiyo vinara ambapo hatujapoteza mechi hata moja tukiwa na alama sita tulizoshinda katika mechi dhidi ya AS Vita na Mabingwa watetezi Al Ahly.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER