Simba yafanya mazoezi kuweka miili sawa

Kikosi chetu kimefanya mazoezi leo jioni katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Beroya hapa Songea kwa ajili ya kuweka miili sawa baada ya safari ndefu.

Kikosi kiliwasili leo saa tano asubuhi hapa Songea kutoka jijini Dar es Salaam na wachezaji wamepewa muda wa kupumzika kabla ya jioni kufanya mazoezi ya kurejesha utimamu wa mwili (recovery).

Wachezaji walipaswa kurejesha miili yao katika utimamu baada ya mchezo wa jana wa ligi dhidi ya Mbeya City katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.

Katika mazoezi hayo mashabiki wengi waliojitokeza waliruhusiwa kushuhudia ambapo walifurahi kuiona timu yao baada ya kupita muda mrefu.

Timu itaendelea na mazoezi kesho na kesho kutwa kabla ya Jumamosi kushuka katika Uwanja wa Majimaji kuikabili Azam FC saa tisa Alasiri.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER