Simba yafanya mazoezi kujiandaa na Kaizer Chiefs

Kikosi chetu kimefanya mazoezi leo jioni katika Uwanja wa Discovery Soccer Park hapa jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini ikiwa ni sehemu ya maandalizi kabla ya kuivaa Kaizer Chiefs Jumamosi Mei 15

Kikosi kimewasili saa tano asubuhi nchini Afrika Kusini kupitia Nairobi ambapo wachezaji walipewa mapumziko kidogo kabla ya kuanza mazoezi jioni ya kuweka miili sawa tayari kwa mchezo huo wa mkondo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hali la hewa ya hapa ni baridi kali na mchezo utakuwa saa 12 jioni kwa saa za huku ambapo nyumbani itakuwa saa moja usiku hivyo tunafanya mazoezi muda huo ili kuwafanya wachezaji wazoee mazingira.

Wachezaji wote wapo vizuri kiafya na wanajitahidi kufuata maelekezo wanayopewa na benchi la ufundi ili kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye mchezo huo.

Licha ya hali ya hewa ya baridi kali tofauti na nyumbani benchi la ufundi linaamini siku tatu za kufanya mazoezi hapa kabla ya mechi zitatosha kuwafanya wachezaji kuzoea mazingira.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER