Simba yafanya mazoezi kuivutia kasi Yanga

Kikosi chetu kimefanya mazoezi leo jioni kujiandaa na mchezo wa fainali ya Michuano ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Yanga utakaofanyika Julai 25, katika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Wachezaji wote wamehudhuria mazoezi na wapo kwenye hali nzuri tayari kwa ajili ya mtanange huo ambao unasubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka ndani na nje ya nchi.

Wachezaji wanafahamu umuhimu wa mchezo huo sababu sio tu kutwaa taji la FA bali pia kuweka heshima ya kushinda makombe mawili msimu huu.

Kikosi kinatarajia kuondoka kesho kuelekea Kigoma tayari kwa mchezo huo wa fainali.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER