Simba yaendeleza ubabe kwa Polisi Tanzania

Kikosi chetu kimeibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Rally Bwalya alitufungia bao hilo muhimu dakika ya 89 kwa mkwaju wa penati baada ya Bernard Morrison kufanyiwa madhambi ndani ya 18 na mlinzi wa Polisi.

Ushindi huu umetufanya kufikisha pointi saba na kusogea nafasi za juu baada ya kucheza mechi tatu ambazo tumeshinda mbili na kutoka sare moja.

Mchezo ulianza taratibu timu zote zikisomana huku tukimiliki sehemu kubwa tukitengeneza nafasi lakini Polisi walikuwa wengi nyuma kuzuia wakati wote.

Kadiri muda ulivyozidi mchezo uliongezeka kasi ambapo Polisi walifanya shambulizi moja hatari dakika ya 44 lakini halikuwa na athari yoyote.

Polisi walimaliza pungufu baada ya mlinzi Juma Ramadhani kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 87 kutokana na kumpiga usoni Bernard Morrison.

Kocha Hitimana Thierry aliwatoa Kibu Denis, Medie Kagere, Erasto Nyoni na Hassan Dilunga na kuwaingiza Bernard Morrison, Mzamiru Yassin, John Bocco na Duncan Nyoni.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER