Simba yaanzia Gym Morocco

Kikosi chetu leo kimeanza rasmi mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi 2021/22 hapa nchini Morocco huku wakianzia gym.

Timu imewasili Morocco jana mchana na wachezaji walipewa mapumziko kabla ya leo kuanza rasmi mazoezi hayo.

Mazoezi hayo yatakuwa ya awamu mbili asubuhi na jioni ili kutengeneza stamina na pumzi kabla ya kuanza kuingia uwanjani kwa ajili ya kujifunza mbinu.

Kambi ya hapa Morocco itakuwa ya wiki mbili ambapo tutarejea nchini siku chache kabla ya kilele cha Simba Day mwishoni mwa mwezi huu.

Kundi la pili la wachezaji ambalo lilibaki Dar es Salaam linatarajiwa kuwasili Morocco muda wowote kutoka sasa na kukamilisha timu nzima na kuendelea na mazoezi pamoja na wenzao.

Leave a comment