Simba yaangukia Shirikisho CAF

Kupoteza kwa mabao 3-1 nyumbani dhidi ya Jwaneng Galaxy kumetufanya kutolewa katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo tutashiriki Kombe la Shirikisho.

Matokeo hayo yametufanya kuwa sawa kwa jumla ya mabao 3-3 lakini Galaxy wanasonga mbele kwa faida ya bao la ugenini kutokana na ushindi wa 2-0 tuliopata kwenye mechi ya kwanza.

Katika mchezo wa leo, tulianza mchezo kwa kasi kwa kuliandama lango la Jwaneng katika dakika 15 za kwanza na kutengeneza nafasi kadhaa ambazo hatukuzitumia vizuri.

Rally Bwalya alitupatia bao la kwanza dakika ya 40 baada ya kuwapiga chenga walinzi waneng na kuachia shuti kali ndani ya 18 lililomshinda mlinda mlango Ezekiel Morake.

Kipindi cha pili Jwaneng walirudi kwa kasi na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 46 kupitia kwa Rudath Wendell baada ya wachezaji kuchelewa kujipanga.

Wendell aliwapatia wageni bao la pili dakika ya 59 kufuatia mpira mrefu wa kurushwa ambao walinzi wetu walizembea kuuondoa.

Dakika ya 85 Gape Mohutsiwa aliwafungia Galaxy bao la tatu kwa kichwa akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Lesego Keredilwe.

Kocha Hitimana Thiery aliwatoa Hassan Dilunga, Taddeo Lwanga, Bernard Morrison na Sadio Kanoute kuwaingiza Peter Banda, Erasto Nyoni, Duncan Nyoni na Meddie Kagere

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER