Simba ya kimataifa zaidi

Timu yetu inarejea katika michuano ya kimataifa ambayo mara nyingi tumekuwa tukipeperusha vema bendera ya nchi ambapao tumekuwa miongoni mwa miamba 10 bora Afrika msimu uliopita.

Leo kikosi kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni kuikabili Red Arrows kutoka Zambia katika mchezo wa kwanza Kombe la Shirikisho Afrika.

Kuelekea mchezo huo maandalizi yamekamilika na wachezaji wote wako kwenye hali nzuri kukahikisha tunapata ushindi mnono nyumbani.

Hakuna majeruhi na wachezaji wote wamefanya mazoezi ya mwisho jana kuelekea mchezo wa leo hivyo benchi la ufundi litakuwa na wigo mpana wa kupanga kikosi.

KOCHA PABLO ATOA NENO

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema anaamini mechi itakuwa ngumu na Red Arrows itajipanga kupata matokeo mazuri ili mechi ya marudiano iwe rahisi kwao lakini sisi tupo tayari kwa mpambano.

Pablo ameongeza kuwa wachezaji wanashika maelekezo yake vizuri na kwa muda mfupi aliokaa nao anaamini tutafanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

“Wachezaji wamekuwa wakiimarika siku hadi siku, katika kipindi hiki kifupi nilichokuwa nao wameonyesha ukomavu mkubwa, ninaamini tutapata ushindi. Tunafahamu mechi itakuwa ngumu lakini tumejiandaa kushinda,” amesema Pablo.

NAHODHA BOCCO

Kwa upande wake Nahodha, John Bocco amesema wachezaji wote wako kwenye hali nzuri na wamejipanga kuhakikisha tunapata ushindi nyumbani na kutorudia makosa yaliyo jitokeza kwenye mechi ya mwisho ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Jwaneng Galaxy.

“Sisi kama wachezaji tupo tayari, tumepata maandalizi mazuri kutoka kwa makocha wetu. Tunajua mchezo utakuwa mgumu Red Arrows sio timu ya kubeza lakini tupo tayari kwa mapambano.

“Tumejifunza kutokana na makosa, tunauchukulia mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy kama funzo kwetu hatutegemei makosa kujitokeza leo,” amesema Bocco.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER