Simba wakali Ngao ya Jamii

Leo saa 11 jioni tutashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kucheza mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga huku tukiwa na historia ya kuchukua mara nyingi kuliko timu yoyote.

Tangu ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2001 tumefanikiwa kuchukua mara tisa na leo kama tutafanikiwa itakuwa mara ya 10.

Ukiacha kuchukua mara tisa pia tumeweka rekodi ya kuchukua Ngao ya Jamii mara nne mfululizo tangu mwaka 2017 hadi mwaka jana.

Mwaka 2017 tulitwaa Ngao ya Jamii kwa kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya kutoka sare ya bila kufungana.

Kuelekea mchezo wa leo nyota wetu watakaocheza kwa mara ya kwanza Derby ya Kariakoo katika kikosi chetu ni Sadio Kanoute, Pape Sakho, Peter Banda, Duncan Nyoni, Henock Inonga Baka, Kibu Denis, Abdulsamad Kassim.

Wengine Israel Patrick, Jimson Mwinuke na Yusuph Mhilu.

Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri kuelekea mechi ya leo isipokuwa Bernard Morrison ambaye amepata maumivu ingawa hata kama angekuwa fiti asingecheza kutokana na kufungiwa mechi tatu.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER