Simba U20 yazidi kutoa dozi Ligi ya Vijana

Timu yetu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 imeendelea kufanya vizuri katika michuano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kuifunga Cambiaso bao moja katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Karume.

Mchezo huo ulikuwa mkali na wa kuvutia muda wote timu zote zikishambuliana kwa zamu na kutengeneza nafasi za kufunga ingawa hawakuzitumia vizuri.

Vijana hao wanaonolewa na Kocha Mussa Mgosi, waliendelea kuonyesha kandanda safi lakini walienda mapumziko wakiwa hawajapata bao.

Dakika ya 78 mshambuliaji Joseph Mbaga alitupatia bao hilo muhimu la ushindi na kutufanya kushinda mchezo wa pili mfululizo kwenye mashindano haya.

Mchezo wetu unaofuata utakuwa dhidi ya JKT utakaopigwa kwenye Uwanja wa Karume, Januari 28 mwaka huu.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER