Simba U20 Washindi wa tatu Michuano ya TFF

Timu yetu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 imefanikiwa kumaliza nafasi ya tatu katika Mashindano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kuifunga JMK Youth bao moja.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku tukiliandama lango la JMK na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini hata hivyo tulikosa umakini katika umaliziaji.

Ambokisie Mwaipopo alitupatia bao hilo la pekee kwa kichwa dakika ya 41 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa JMK.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kushambulia huku tukitengeneza nafasi nyingi ambazo hazikuweza kubadili ubao wa matokeo.

Kabla ya kufungwa na Azam katika mchezo wa nusu fainali kikosi chetu kilikuwa kimeshinda mechi zote nne katika hatua ya makundi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER