Baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na Michuano ya Azam Sports Federation Cup, Simba sasa inajipanga kunyakua Ligi ya Mabingwa Afrika ndani ya miaka miwili ijayo.
Kauli hii imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’ muda mfupi baada ya kutwaa ubingwa wa FA kwa kuifunga Yanga katika Uwanja wa Lake Tanganyika.
Try Again amesema kwa sasa Simba ni timu kubwa na inapaswa kuwaza mambo makubwa na ndiyo maana tunajipanga ndani ya miaka miwili ijayo kutwaa ubingwa wa Afrika.
“Simba ni timu kubwa na ndani ya miaka miwili tunajipanga kuchukua Ubingwa wa Afrika lazima tuwaze vitu vikubwa ili kuwa wakubwa,” amesema Try Again.
Kuhusu usajili wa msimu ujao Try Again amesema tunasubiri ripoti ya Kocha Didier Gomes ili kuangalia watu gani wakuongeza na wakupunguza.
2 Responses
Nguvu Moja
Simba nguvu moja