Simba Queens yatolewa michuano ya Cecafa

Kikosi chetu cha Timu ya Wanawake Simba Queens imetolewa kwenye Michuano ya Caf Women’s Champions League Cecafa Qualifiers 2021 baada ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji Vihiga Queens katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Nyayo.

Mchezo huo haukuanza kwa kasi huku walimu wa timu zote wakiwataka wachezaji wao kuchukua tahadhari mara zote hali iliyosababisha mashambulizi kuwa machache na mpira kuchezwa zaidi kati kati ya kiwanja.

Kipindi cha pili timu zote ziliingia kwa nia ya kutafuta bao na wenyeji Vihiga walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 63 lililofungwa na Maurine Achieng.

Aisha Juma alitusawazishia bao hilo dakika ya 69 baada ya mpira mrefu uliopigwa Danai Bhoho kumkuta Mawete Musolo aliyepiga krosi safi iliyomkuta mfungaji.

Vihiga walipata bao la ushindi dakika ya 88 kupitia kwa Jentrix Shikangwa baada ya kumalizia mpira wa kona.

Kocha wetu Hababuu Ally, aliwatoa Violeth Nicholaus ambaye alipata maumivu na Ruth Kipoi na kuwaingiza Aisha Juma na Maimuna Kaimu.

Baada ya kushindwa kuingia fainali kikosi chetu kitacheza mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu Septemba 9, na timu itakayopoteza kati ya Lady Doves au Commercial Bank of Ethiopia ambao wapo uwanjani kucheza nusu fainali ya pili.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER