Simba Queens yapaa kuelekea Ethiopia

Kikosi chetu cha Simba Queens kimeondoka nchini kuelekea Ethiopia kwa ajili ya kushiriki michuano ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Simba Queens imeondoka na kikosi kamili cha wachezaji 24 tuliowasajili kwa ajili ya msimu wa mashindano 2024/25 chini ya Kocha Juma Mgunda.

Kikosi kimeondoka huku wachezaji wakiwa na morali ya kwenda kufanya vizuri ili kutwaa ubingwa huo ambao utatupa tiketi ya kuiwakilisha CECAFA kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika.

Kikosi kitafika Ethiopia siku mbili kabla ya kuanza michuano ili kuwapa wachezaji muda wa kuzoea mazingira na hali ya hewa.

Mchezo wetu wa kwanza utakuwa Jumamosi dhidi ya AFAD Djibouti kutoka Djibouti.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER