Simba Queens yakabidhiwa kombe lake

Timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens, imekabidhiwa taji lake la Ubingwa wa Ligi (Serengeti Lite Women Primier League) baada ya kumalizika mchezo maalumu dhidi ya Twiga Stars leo.

Baada ya mchezo huo maalumu uliofanyika Uwanja wa Uhuru fursa ya kukabidhiwa ubingwa umemalizika kwa kupoteza mabao 2-1.

Bao letu pekee kwenye mchezo huo limefungwa na kinara Oppa Clement dakika ya 81.

Simba Queens imemaliza Ligi ya Wanawake ikiwa na pointi 51 ikicheza mechi 19 na kushinda 16 huku ikitoka sare tatu.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. URAMBO TABORA hongeren kwa ubingwa huu wa ligikuu ya wanawake mwenyezi MUNGU awazidishie neema na baraka zilizo Zaid kaita mashindano ya CECAFA muweze kupata ushindi Tena AMIN

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER