Timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens leo imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ukonga Boys U15 katika mchezo wa kirafiki ikiwa ni maandalizi ya michuano ya CAF Women Champions Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Jakaya Kikwete Youth Park, ulikuwa mkali lakini Simba Queens ilitawala kwa kiasi kikubwa.
Hadi mapumziko tulikuwa mbele kwa mabao mawili yaliyofungwa na Ruth Kipoyi na Danai Bhobho.
Mariam Nasri aliipatia Simba Queens bao la tatu lililohitimisha karamu ya mabao.
Kikosi cha Simba Queens kitaondoka Jumatano kuelekea nchini Kenya tayari kwa michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Agosti 28 mwaka Huu.
GROUP A
Simba Queens (Tanzania)
Lady Doves WFC (Uganda)
PVP FC (Burundi)