Simba Queens yailaza na viatu Yanga Princess, yapaa kileleni

Timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens imekaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake (Serengeti Lite Women Premier League) baada ya kuwachakaza bila huruma Yanga Princess mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Uhuru.

Mchezo ulianza kunoga dakika ya 30 baada ya Nahodha Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’ kutupatia bao la kwanza kwa shuti kali nje ya 18 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Joelle Bukuru.

Oppa Clement alitupatia bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 42 baada ya mlinzi wa kati Happyness Mwaipaja kuunawa makusudi mpira uliokuwa unaingia wavuni na kuonyeshwa kadi nyekundu.

Joelle Bukuru alipiga bao la tatu dakika ya 50 kwa shuti la mguu wa kushoto lililomshinda mlinda mlango wa Yanga Princess, Husna Zuberi.

Ushindi huo unatufanya kufikisha alama 39 tukiwazidi Yanga alama moja baada ya wote kucheza mechi 15.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER