Simba Queens yaichakaza Yanga Princess

Kikosi chetu cha Timu ya Wanawake Simba Queens, kimeibuka na ushindi mabao 4-1 dhidi ya Yanga Princess katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League) uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Asha Djafar alitufungia bao la kwanza dakika ya saba kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 akimalizia mpira wa krosi uliopigwa kutoka upande wa kulia.

Oppah Clement alitupatia bao la pili kwa kichwa dakika ya 53 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Asha Djafar.

Oppah aliongeza bao la tatu dakika ya 70 baada ya kumpiga chenga mlinda mlango wa Yanga, Zulfa Makao kufuatia kupokea pasi safi kutoka kwa Zena Khamis.

Aisha Masaka aliipatia Yanga bao la kwanza kwa mkwaju wa penati dakika ya 77 baada ya Violeth Nicholas kumfanyia madhambi Amina Bilal.

Asha Djafar alitufungia bao la nne kwa shuti kali la mguu wa kushoto dakika ya 80 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Oppah.

Ushindi wa leo unatufanya kufikisha alama 12 baada ya kushinda mechi zote nne huku tukiwa na mabao 31, ya kufunga.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER