Simba Queens yaichakaza Mlandizi

Kikosi chetu cha Simba Queens kimeendelea kutoa dozi nene kwa kila timu inayokutana nayo kwenye Ligi Kuu ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League) baada ya kuifunga Mlandizi Queens mabao 3-0 mchezo uliopigwa Uwanja wa Mo Simba Arena.

Fallone Pambani alitupatia bao la kwanza dakika ya 32 kabla ya Opa Clement kuongeza la pili dakika ya 45 na kutufanya kwenda mapumziko tukiwa mbele kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na ilituchukua dakika 10 kupata bao la tatu lililofungwa tena na Opa kwa mkwaju wa penati baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Baada ya bao hilo tuliendelea kuliandama lango la Mlandizi huku tukitengeneza nafasi za kufunga ingawa hatukuzitumia vizuri.

Kocha Sebastian Nkoma aliwatoa Olaiya Barakat, Sabina Thom na Pambani na kuwaingiza Amina Ramadhani, Mercy Tagoe na Jackline Albert.

Ushindi huo umetufanya kufikisha pointi 24 baada ya kushinda mechi zote nane tulizocheza hadi sasa.

SHARE :
Facebook
Twitter

3 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER