Simba Queens yaichakaza JKT 7-0

Timu yetu ya Simba Queens imeendelea kuwa moto wa kuotea mbali katika Ligi ya Wanawake ya (Serengeti Lite Women’s Premier League) baada ya kuichakaza bila huruma JKT Queens mabao 7-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Mo Simba Arena.

Kinara wa ushambuliaji Opa Clement, alitupatia bao la kwanza mapema dakika ya pili kabla ya Joelle Bukuru kuongeza la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 19.

Opa aliongeza bao la tatu dakika ya 30 kabla ya Pambani Kuzoya na Jackline Albert kutupia moja kila mmoja na kutufanya kwenda mapumziko tukiwa mbele kwa mabao 5-0.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na ilituchukua dakika tatu tu kupata bao la sita lililofungwa na Pambani kabla ya Asha Djafar aliyetokea benchi kupiga la saba.

Kocha Sebastian Nkoma aliwatoa Sabina Thom, Olaiya Barakat, Jackline Albert na kuwaingiza Amina Ramadhan, Asha Djafar na Mercy Tagoe.

Ushindi wa leo unatufanya kuendelea kubaki kieleleni mwa msimamo tukiwa na alama 27 baada ya kushinda mechi zote tisa tulizocheza.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER