Simba Queens yaenda Kenya kushiriki michuano ya CAF

Kikosi cha timu yetu ya Wanawake Simba Queens, kimeondoka alfajiri kuelekea nchini Kenya kikiwa na wachezaji 22 tayari kushiriki michuano ya CAF Women Champions Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) itakayoanza Jumamosi Agosti 28.

Simba Queens imepata nafasi ya kushiriki michuano hiyo baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Wanawake ‘Serengeti Lite Premier League’ msimu uliopita.

Timu hiyo iliyo chini ya Kocha Habab Ally itacheza mechi yake ya kwanza Jumamosi Agosti 28, saa 10 jioni katika Uwanja wa Nyayo dhidi ya PVP FC.

Kikosi kamili kilichosafiri

Makipa

Gelwa Yona Lugomba, Janeth Shija Simba, Zubeda Mohamed Mgunda

Mabeki

Dotto Evarist, Fatuma Issa, Julitha Singano, Maimuna Kaimu,Sylvia Thomas, Violeth Nicholaus, Violeth Thadeo, Wema Richard

Viungo

Danai Bhobho, Jackline Albert, Joelle Bukuru, Kadosho Shabani, Koku Ally, Zena Khamis,

Washambuliaji

Aisha Juma, Asha Djuma, Flaviana Mawete, Ruth Kipoyi, na Shelder Boniface

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER