Simba Queens yaanza kutoa dozi Kenya

Timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens imeanza vema michuano ya Caf Women’s Champions League Cecafa Qualifiers 2021 baada ya kuifunga PVP FC Buyenzi kwa mabao 4-1  katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Tulianza mchezo kwa kasi ambapo tulipata bao la kwanza dakika ya pili kupitia kwa Danai Bhobho baada ya kupiga mpira wa mbali uliomshinda mlinda mlango wa PVP.

Mawete Musolo alitupatia bao la pili dakika ya 32 kabla ya Nicole Igilima kuiingiza PVP bao la kusawazisha na kufanya timu kwenda mapumziko tukiwa mbele kwa mabao 2-1.

Mawete alitupatia bao la tatu kwa mkwaju wa penati dakika ya 81 kabla ya Aisha Juma kumalizia la nne dakika mbili kabla ya mchezo kumalizika.

Kocha Habab Ally aliwatoa Asha Djafar na Janeth Shija na kuwaingiza Aisha Juma na Zubeda Mgunda.

Simba Queens itacheza mchezo wa pili Agosti 31 katika Uwanja wa Moi Kasarani dhidi ya Lady Doves.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER