Kikosi cha timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens itakutana na Lady Doves katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano ya Caf Women’s Champions League Cecafa Qualifiers 2021 utakaopigwa Uwanja wa Nyayo, Septemba 9 saa saba mchana.
Timu hizo zilikuwa kundi A ambapo tulipokutana mchezo ulikuwa mkali na ulimalizika kwa sare ya bila kufungana na kutinga nusu fainali.
Jana tulipoteza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Vihiga Queens ya Kenya wakati Lady Doves wamefungwa na Commercial Bank of Ethiopia kwa mikwaju ya penati 5-4.
Up
Mchezo huo utakuwa ni wa kukata ngebe kutokana na mechi ya kwanza kwenye hatua ya makundi kumaliza kwa sare ambapo lazima mshindi apatikane.