Simba Queens, Lady Doves hakuna mbabe

Kikosi chetu cha Timu ya Wanawake ya Simba Queens, kimetoka sare ya bila kufungana na Lady Doves ya Uganda katika mchezo wa pili wa Michuano ya Caf Women’s Champions League Cecafa Qualifier 2021 uliopigwa Uwanja wa Moi Kasarani, jijini Nairobi.

Mchezo huo ulianza kwa kasi timu zote zikishambuliana kwa zamu kuhakikisha wanapata bao la uongozi ili kujiweka salama.

Washambuliaji wetu Mawete Musolo na Oppa Clement walipoteza nafasi kadhaa ambazo zingetufanya kwenda mapumziko tukiwa mbele kwa zaidi ya mabao mawili.

Kipindi cha pili timu zote zilirudi kwa kasi kila moja ikitafuta bao lakini milango iliendelea kuwa migumu huku safu za ulinzi zikifanya kazi zao ipasavyo.

Kocha Hababuu Ally aliwatoa Ruth Kipoyi na Zena Khamis na kuwaingiza Aisha Juma na Asha Djafar.

Baada ya mchezo wa leo kikosi chetu kitashuka tena dimbani Septemba 3, dhidi ya FAD FC saa saba mchana katika mchezo wa mwisho wa kundi A kwenye Uwanja wa Moi Kasarani.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER