Simba Queens kuweka rekodi 2022

Kocha Mkuu wa Simba Queens, Sebastian Nkoma amesema lengo letu ni kuhakikisha tunatwaa taji la Ligi ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League) kwa mara ya tatu mfululizo na kuweka rekodi.

Nkoma amesema hadi sasa tumeshinda mechi zote saba tulizocheza na inaonyesha kikosi kiko imara hivyo tunaweza kufikia malengo yetu.

Akizungumzia mchezo wa kesho dhidi ya Mlandizi Queens, Nkoma amesema utakuwa mgumu lakini tuko imara kuhakikisha tunaendeleza wimbi la ushindi.

“Tumejipanga kuweka rekodi ya kuchukua taji hili kwa mara tatu mfululizo. Tayari tumechukua mara mbili na malengo ni kuchukua tena msimu huu.

“Kikosi kiko vizuri kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Mlandizi. Tunajua utakuwa mchezo mgumu lakini tumejipanga kuondoka na alama zote tatu,” amesema Nkoma.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER