Simba Queens kuendelea walipoishia

Nahodha wa timu yetu ya Wanawake Simba Queens, Violeth Nicholaus amesema tutaendelea tulipoishia kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Yanga Princess utakaopigwa Uwanja wa Mkapa saa 10:00 jioni.

Nahodha huyo ameongeza kuwa kama tulivyofanya kwenye mchezo uliopita tulipokutana ambao tuliibuka na ushindi wa mabao 3-0 ndipo tutakapoendelea napo.

Violeth amesema maandalizi yamekamilika na matumaini ya kuibuka na ushindi ni makubwa licha ya mchezo kuwa mgumu kutokana na Yanga ambao watataka kujitahidi ili kufuta uteja.

“Tupo kamili, wachezaji tuko kwenye hali nzuri. Tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini tutapambana kupata ushindi. Tutaendeleza tulipoishia,” amesema Violeth.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER