Simba Queens kuanza maandalizi ya msimu kesho

Kikosi cha Simba Queens kinatarajia kuanza maandalizi kesho Alhamisi ya michuano ya klabu Bingwa kwa ukanda wa Afrika Mashariki na kati CECAFA.

Akizungumza na Simba App Kocha wa Queens, Mussa Hassan Mgosi amesema wachezaji wote wanawasili kambini leo na kesho waanza rasmi programu ya mazoezi

Mwalimu Mgosi amesema atakuwa na mazoezi ya Uwanjani, Beach pamoja na Gym ili kutengeneza kikosi imara kuelekea michuano ya CECAFA.

“Tunaanza maandalizi ya msimu kesho, na wachezaji wote wanatakiwa kuingia kambini leo ili programu yetu iende kama tulivyopanga,” amesema Mgosi.

Simba Queens itashiriki mashindano ya klabu bingwa kwa ukanda wa CECAFA yanayotaraji kuanza Agosti 14 mwaka huu nchini Ethiopia ambapo Bingwa wa michauno hiyo anapata tiketi ya kushiriki mashidano ya klabu Bingwa Afrika.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER