Simba Queens haipoi, haiboi

Timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens imeendelea kutoa dozi katika Ligi ya Wanawake (Serengeti Women’s Premier League) baada ya kuichapa Alliance Girls mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Mchezo huo ulikuwa mgumu timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini milango ilikuwa migumu na tulienda mapumziko tukiwa hatujafungana.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi na kuliandama lango la Alliance ambapo kinara Oppah Clement alitufungia mabao ya haraka dakika ya 82 na 84 na kutuhakikishia alama tatu muhimu ugenini.

Kocha Sebastian Nkomwa alifanya mabadiliko mawili ya kuwatoa Olaiya Barakat na Jackline Albert na kuwaingiza Falone Pambani pamoja na Sabinah Thomas.

Ushindi wa leo umetufanya kufikisha pointi 15 tukiendelea kushikilia usukani baada ya kucheza mechi tano na kushinda zote tukifunga mabao 33 na kufungwa mawili.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER