Simba Queens haikamatiki, haishikiki

Timu yetu ya Simba Queens imeendelea kufanya vizuri katika Ligi ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League) baada ya kuifunga Baobab Queens mabao 3-1 leo katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.

Olaiya Barakat alitufungia bao la kwanza dakika ya 10 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Baobab na kupiga shuti lililomshinda mlinda mlango wao.

Baada ya bao hilo tuliendelea kuliandama lango la Baobab huku nao wakifanya mashambulizi machache ingawa hayakuwa na madhara.

Opa Clement alitupatia bao la pili dakika ya 60 kwa shuti kali ndani ya 18 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopgiwa na Asha Djafar.

Zainabu Rashid aliwafungia Baobab bao la kufutia machozi dakika ya 72 kwa mkwaju wa penati.

Asha Djafar alitupatia bao la tatu dakika ya 80 na kukamilisha karamu ya mabao na kutupatia pointi tatu muhimu.

Kocha Sebastian Nkoma aliwatoa Olaiya, Dotto Evarist, Aisha Juma na Asha Djafar na kuwaingiza Sabina Thom, Maimuna Khamis, Amina Ramadhani na Pambani Kozoya.

Ushindi huo umetufanya kufikisha pointi 30 na kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo baada ya kushinda mechi zote 10.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER