Simba, N Card watatua tatizo la tiketi Simba Day

Viongozi wa Simba na wasimamizi wa mfumo wa tiketi za kielektroniki N Card, wamekubaliana kutoa kadi nyingine tofauti kwa ajili ya watu kuingia uwanjani kwenye Tamasha la Simba Day.

Viongozi hao wamekutana kwa dharura kutatua tatizo la upatikanaji wa tiketi hizo baada ya kadi za kawaida za N Card kumalizika kwenye vituo vya mauzo hatua iliyosababisha usumbufu mkubwa kwa mashabiki na wapenzi wa Simba

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez, aliyeongoza kikao hicho cha dharura ofisini amesema kwa sababu ya mwafaka uliofikiwa, kadi mpya zitakuwa zimesambazwa katika vituo vyote katika muda wa saa moja kutoka sasa.

“Nawaomba washabiki na wanachama wa Simba wawe watulivu na wavumilivu katika wakati huu. Jambo hili limefanyiwa kazi na sasa tiketi zitaanza kuuzwa kama kawaida kuanzia leo jioni,” amesema.

Tiketi hizo mpya zitakuwa zikiuzwa katika vituo vyote 16 vilivyotangazwa kuuza tiketi za Simba Day jijini Dar es Salaam.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. Hi, I do think your web site may be having browser
    compatibility problems. When I take a look at your website in Safari, it looks
    fine however, if opening in Internet Explorer,
    it has some overlapping issues. I merely wanted to give you
    a quick heads up! Apart from that, wonderful site!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER