Kikosi chetu kimeendeleza wimbi la ushindi katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kuichakaza Dodoma Jiji mabao 3-1 katika mtanange uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji Chris Mugalu alitupatia bao la kwanza mapema dakika ya nane baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Rally Bwalya
Dakika ya 29 Dodoma ilisawazisha bao hilo kupitia kwa Cleophas Mkandala kufuatia mpira wa kona uliopigwa na Anuari Jabir uliomponyoka mlinda mlango Aishi Manula.
Luis Miquissone alitupatia bao la pili dakika ya 55 baada ya kumalizia pasi iliyopigwa kiufundi na Clatous Chama.
Mugalu aliongeza bao la tatu dakika ya 67 kwa shuti kali la chini chini akiwa ndani ya 18 kufuatia kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Chama.
Kocha Didier Gomez aliwatoa Mzamiru Yassin, Miquissone na Mugalu na kuwaingiza Bernard Morrison, Ibrahim Ajibu na Medie Kagere.
Ushindi wa leo unakuwa wa tano mfululizo baada ya kuzifunga timu za Mtibwa, Mwadui, Kagera Sugar, Gwambina na leo Dodoma ambapo tumefikisha alama 61 tukiendelea kusalia kileleni.
One Response
Mimi sipendi pale timu imeshajiakikishia ushindi inaaza kupooza mpira nikushambulia tu kamavile atujashinda