Simba, Mtibwa hakuna mbabe

Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar uliopigwa Uwanja wa Manungu Complex mkoani Morogoro umemalizika kwa sare ya bila kufungana.

Mchezo ulianza taratibu timu zikisomana huku zikitumia mipira ya juu kutokana na uwanja kuteleza baada ya mvua kubwa kunyesha usiku wa kuamkia leo.

Dakika ya 45 tulifanya shambulio kali langoni mwa Mtibwa baada ya shuti kali lililopigwa na Hassan Dilunga kupaa mita chache akimalizia pasi ya kichwa iliyopigwa na Pape Sakho.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi na kutengeneza nafasi za kufunga lakini bahati haikuwa upande wetu.

Kocha Pablo Franco aliwatoa Hassan Dilunga, Chris Mugalu, Mzamiru Yassin, Gadiel Michael na Henock Inonga na kuwaingiza Clatous Chama, Bernard Morrison, Mohamed Hussein, Kennedy Juma na John Bocco.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER