Simba, Mlandege Hakuna Mbabe

Licha ya kupata sare ya bila kufungana dhidi ya Mlandege tumefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Michuano ya Mapinduzi inayoendelea Visiwani Zanzibar.

Matokeo haya yametufanya kufikisha alama nne na kuwa kinara wa kundi C.

Mchezo ulianza kwa kasi ya kawaida huku mashambulizi yakiwa machache kutoka kwa timu zote.

Kipindi cha pili kasi iliongezeka kiasi huku tukipoteza nafasi mbili za wazi ambazo zingetufanya kupata mabao.

Kocha Pablo Franco aliwaingiza David Udoh, Cheick Mukoro, Bernard Morrison, Shomari Kapombe na Medie Kagere na kuwatoa Yussuf Mhilu, Chris Mugalu, Pape Sakho, Kibu Denis na Gadiel Michael.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER