Simba mguu mmoja ndani makundi Afrika

Ushindi wa mabao 2-0 tuliopata ugenini dhidi ya Jwaneng Galaxy nchini Botswana umetufanya kuzidi kusogelea hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Matokeo ya leo yanatufanya kuhitaji ushindi, sare ya aina yoyote au kufungwa bao moja ili kupata tiketi ya kuingia hatua ya makundi.

Kiungo Taddeo Lwanga alitufungia bao la kwanza mapema dakika ya pili baada ya walinzi wa Galaxy kuzembea kuondoa hatari kufuatia mpira wa kona uliopigwa na Rally Bwalya.

Dakika tatu baadae nahodha John Bocco alitupatia bao la pili kwa shuti kali ndani ya 18 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Bwalya aliyepokea pasi ya kona iliyopigwa na Bernard Morrison.

Dakika tano za kipindi cha pili wenyeji Galaxy walifanya mashambulizi langoni kwetu lakini idara ya ulinzi ilikuwa makini kuwakabili na kuhakikisha nyavu zetu haziguswi.

Kocha Hitimana Thiery aliwatoa Bwalya, Sadio Kanoute, Bocco na Morrison kuwaingiza Erasto Nyoni Mzamiru Yassin, Duncan Nyoni na Medie Kagere.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER