Simba macho yote kwa KMC

Baada ya kupoteza mchezo uliopita sasa nguvu zote tumezielekeza katika mchezo wa kesho wa Ligi Kuu dhidi ya KMC utakaopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Alama tatu katika mchezo wa kesho zitatufanya kuwa karibu na ubingwa na tutahitaji sare kwenye mechi ya Coastal Union ili kutawazwa mabingwa wapya wa ligi kuu kwa mara ya nne mfululizo.

Kocha msaidizi, Seleman Matola amesema wachezaji wote wapo kambini na maandalizi yamekamilika kwa kiasi kikubwa huku matumaini ya ushindi yakiwa makubwa.

Matola ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu sababu ligi inaelekea ukingoni na kila timu ikitaka kijikwamua kutoka nafasi iliyopo lakini tunaamini tutaondoka na alama zote tatu.

“Ligi inaelekea ukingoni na kila timu inataka kumaliza kwenye nafasi nzuri zaidi, sisi tunataka ubingwa na tukishinda tutakuwa tumekuwa mabingwa sababu wanaotufuata wakishinda mechi zao tutakuwa sawa lakini idadi ya mabao tumewaacha mbali,” amesema Matola.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER