Simba kutua Kanda ya Ziwa na nyota 28

Kikosi chetu kitaondoka leo jioni kwa ndege kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa ajili ya mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom kikiwa na wachezaji wote 28 waliosajiliwa msimu huu.

Kocha Didier Gomez na wasaidizi wake, wameamua kuondoka na kikosi kizima kutokana ugumu wa mechi huku timu zote zikiwa zimejipanga kipindi hiki cha lala salama ligi ikielekea ukingoni.

Ratiba ya michezo hiyo Kanda ya Ziwa itaanza Jumapili ambapo tutashuka kwenye Uwanja wa Kambarage Shinyanga kuikabili Mwadui na siku tatu baadae (lini?) tutaenda Kaitaba kuifuata Kagera Sugar na mchezo wa mwisho utakuwa dhidi ya Gwambina utakaopigwa Uwanja wa Gwambina, Aprili 24.

Kikosi Kamili kitakachokwenda Kanda ya Ziwa;

Makipa

Aishi Manula
Beno Kakolanya
Ally Salim

Mabeki

Shomari Kapombe
Joash Onyango
Pascal Wawa
Ibrahim Ame
Erasto Nyoni
Gadiel Michael
Mohamed Hussein
Kennedy Juma
David Kameta

Viungo

Jonas Mkude
Rally Bwalya
Said Ndemla
Mzamiru Yassin
Luis Miquissone
Hassan Dilunga
Clatous Chama
Bernard Morrsion
Francis Kahata
Taddeo Lwanga

Washambuliaji

Medie Kagere
John Bocco
Ibrahim Ajib
Kope Mugalu
Miraji Athumani
Perfect Chikwende

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER