Simba kutorudia makosa kwa Red Arrows

Nahodha wa timu John Bocco, amesema maandalizi kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows yamekamilika na wachezaji wamejipanga kuhakikisha hawarudii makosa.

Amesema tumejifunza katika mchezo uliopita wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy na hatuwezi kurudia makosa yale malengo ni kutinga hatua ya makundi.

“Tumeiangala Red Arrows kupitia mkanda wa video ni timu nzuri na tunajua nao wametufuatilia lakini tumejidhatiti kuhakikisha tunashinda.

“Sisi wachezaji tupo tayari, tumepata maandalizi mazuri kutoka kwa makocha wetu. Tunajua mchezo utakuwa mgumu Red Arrows si timu ya kubeza lakini tuko tayari kwa mapambano.

“Tumejifunza kutokana na makosa, tunauchukulia mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy kama funzo kwetu hatutegemei makosa yale kujitokeza tena Jumapili,” amesema Bocco.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER