Simba kusaka pointi tatu nyingine za Kanda ya Ziwa leo

Kikosi chetu leo kitaendelea kampeni ya kusaka pointi tatu kwenye mechi zetu za Kanda ya Ziwa ambapo leo tutashuka katika Uwanja wa Kaitaba kuikabili Kagera Sugar saa 10 jioni.

Kampeni za kusaka pointi tatu za Kanda ya Ziwa zilianza wiki iliyopita katika Uwanja wa CCM Kambarage tulipoibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya Mwadui FC.

Kocha msaidizi, Suleiman Matola amesema anatarajia mchezo utakuwa mgumu na anaiheshimu Kagera hasa baada ya kupata kocha mpya, Francis Baraza lakini tumejipanga na tunahitaji kupata alama zote tatu.

Amesema maandalizi ya mchezo yamekamilika na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na walifanya mazoezi ya mwisho jana kujiandaa na mechi ya leo.

TAARIFA YA KIKOSI

Kiungo Bernard Morrison pekee ndiye atayekosa mchezo wa leo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano wengine wote wapo tayari kwa mchezo.

MCHEZO ULIOPITA

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Kagera Sugar uliopigwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Novemba, 4 mwaka jana tuliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Katika mchezo huo mabao yetu yalifungwa na Nahodha John Bocco kwa penati na kiungo Said Ndemla.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER