Kikosi chetu leo kitaanza mazoezi kujiandaa na mchezo ujao wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Novemba 19, Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Timu itaanza mazoezi ya Gym asubuhi na jioni itafanya uwanjani ili kurudisha utimamu wa mwili kwa wachezaji baada ya kupewa mapumziko ya siku nne.
Wachezaji watakuwa wanafanya mazoezi na kurudi nyumbani kwa sababu timu bado haijaingia kambini moja kwa moja.
Wachezaji watakaoanza mazoezi ni wale ambao hawajaitwa katika vikosi vyao vya timu za taifa zinazojiandaa na mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Dunia.
One Response