Simba kurejea Dar kesho

Baada ya kukamilika kwa kambi ya mazoezi ya wiki mbili mkoani Arusha kikosi chetu kesho saa mbili usiku kitarejea jijini Dar es Salaam tayari kwa Tamasha la Simba Day Jumapili.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu, Ezekiel Kamwaga amesema kambi ya Arusha imeenda vizuri na benchi la ufundi limeridhika na viwango vya wachezaji.

Kamwaga amesema baada ya kufika jijini kikosi kitaingia kambini moja kwa moja kujiandaa na tamasha kubwa ya kihistoria la Simba Day, Septemba 19 ambalo mwaka huu litakuwa la tofauti.

“Kambi ya wiki mbili jijini Arusha imemalizika na kesho usiku kikosi kitarudi mjini tayari kwa Simba Day na maandalizi yote yamekamilika,” amesema Kamwaga.

Kuhusu zoezi la kununua tiketi mtandaoni kusumbua Kamwaga amesema uongozi unaendelea kupambana kuhakikisha linamalizika na kila Mwanasimba anapata nafasi ya kushuhudia tamasha hilo la kihistoria.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER