Simba kupumzisha baadhi ya nyota, kuwapa nafasi wengine

Baada ya kujihakikishia kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mara ya nne mfululizo Kocha Mkuu, Didier Gomes amesema atawapumzisha baadhi ya wachezaji waliotumika sana na kuwapa nafasi wengine.

Gomes amewataja nyota hao Miraji Athuman, Said Ndemla, Gadiel Michael na David Kameta kuwa wanafanya vizuri mazoezini na anafurahi kufanya nao kazi lakini kutokana na ukubwa wa kikosi wameshindwa kupata nafasi.

Gomes amesema msimu ulikuwa mrefu na wachezaji walipambana na kufanikisha tunatetea ubingwa hivyo kwenye mechi tatu za ligi zilizosalia atawapa nafasi nyota wengine ambao hawajacheza mara nyingi.

“Tunashukuru tumefanikiwa kutetea ubingwa wetu, nadhani tutawapumzisha wachezaji waliocheza mechi nyingi na kuwapa nafasi wengine sababu msimu ulikuwa mrefu.

“Katika mechi tatu za ligi zilizobaki tutawapa nafasi wachezaji ambao hatukuwatumia sana. Simba ni familia ukipanga kikosi bado unakuwa na wachezaji 10 ambao ni bora lakini wanakosa nafasi hivyo ni wakati wao huu,” amesema Gomes.

Baada ya ushindi wa mabao 2-0 tuliopata jana dhidi ya KMC tumejihakikishia kutetea ubingwa kufuatia kufikisha alama 76 ambazo zinaweza kufikiwa na anayetufuatia lakini tumemzidi uwiano wa mabao ya kufunga.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

  1. NI Jambo zuri sana kuwapumzisha wachezaji waliotumika Sana kwa kuzingatia hapo kesho Kuna CAF SUPER LEAGUE.
    Hii no nafasi ya akina AJIBU,KAKOLANYA,CHIKWENDE,MIRAJI,NDEMLA,GADIEL,DUCHU,KIMETA n.k kuonesha stadi zao.

  2. Nawapongeza viongozi wa simba na team zote kwa ujumla,,kwa kuwa wamoja na wenye kupendana .hasa kama shabiki halali na nisiyeyumbishwa .tarehe 25 naomba tuchomoe betri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER