Simba kupambana dhidi ya Kaizer hadi kieleweke

Kiraka Erasto Nyoni amesema mchezo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs utakaopigwa Jumamosi Mei 15, mwaka huu katika Uwanja wa FNB, jijini Johannesburg  utakuwa mgumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri kwa namna yoyote.

Erasto amesema hali ya hewa ya Afrika Kusini ni baridi kali lakini hawatakubali iwe kigezo cha kushindwa kupata matokeo mazuri dhidi ya Kaizer.

Nyota huyo ameongeza kuwa wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na morali ipo juu watapambana kuhakikisha Jumamosi tunapata ushindi.

“Kwa namna yoyote tutahakikisha tunapambana kupata matokeo mazuri, hali ya hewa ni baridi kali lakini haitakuwa kikwazo kwetu kushindwa kupata ushindi,” amesema Erasto.

Erasto amewaomba Wanasimba kote duniani kuendelea kuwaombea ili wawe salama kabla ya mchezo ili kufanikisha malengo yetu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER