Simba kupaa jioni kuifuata Biashara Mara

Kikosi chetu leo saa 12 jioni kitasafiri kwa ndege kuelekea jijini Mwanza kabla ya kwenda Mara tayari kwa mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Biashara United utakaopigwa Jumanne Septemba 28 katika Uwanja wa Karume.

Baada ya kuwasili jijini Mwanza timu italala hapo kisha safari ya kuelekea mkoani Mara itaanza kesho asubuhi.

Licha ya kushindwa kuchukua Ngao ya Jamii jana bado hatujatetereka na malengo yetu ni yale yale kutetea ubingwa wa ligi pamoja na michuano ya Azam Sports Federation Cup.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER