Simba yapaa Misri kuifuata Al Ahly

Kikosi kimeondoka nchini muda huu kuelekea Misri kwa ajili ya mchezo wa mwisho hatua ya makundi Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.

Mechi hiyo  itachezwa Ijumaa, Aprili 9 saa nne usiku kwa saa za Tanzania.

Timu imeondoka na wachezaji 26 ikipitia Dubai kabla ya kwenda Misri tayari kwa mchezo huo ambao hautabadili wala kuathiri chochote kwenye msimamo wa kundi letu tukifanikiwa kumaliza kileleni.

Meneja wa timu, Patrick Rweyemamu amesema kikosi kimefanya mazoezi ya mwisho leo asubuhi kwenye viwanja vya Mo Simba Arena na maandalizi ya safari yamekamilika.

“Timu inaondoka leo saa 9 alasiri ikiwa na wachezaji 25 na itapitia Dubai kabla ya kuelekea Misri tayari kwa mchezo wetu wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Al Ahly utakaopigwa siku ya Ijumaa,” amesema Rweyemamu.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER