Simba kumalizia kambi Arusha

Kikosi cha wachezaji 23 na viongozi 11 wa Simba, kitaondoka jijini Dar es Salaam kesho kuelekea Arusha kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa mashindano.

Akizungumza na Simba App leo, Meneja wa Timu ya Simba, Patrick Rweyemamu amesema kikosi hicho kitakaa Arusha hadi kitakaporejea Dar es Salaam kucheza wakati wa Tamasha la Simba Day Septemba 19 mwaka huu.

“Kikosi hicho cha wachezaji 23 kinajumuisha wachezaji wa kikosi cha kwanza na wachache wa timu ya vijana ambao mwalimu anataka kuwaona kwenye mazoezi.

” Tunatarajia wachezaji walio katika timu za taifa watakuja kujiunga na wenzao mara watakapomaliza majukumu yao ya timu za taifa,” amesema Rweyemamu.

Takribani wachezaji 13 wa Simba wameitwa katika timu tofauti za taifa kwa ajili ya mashindano ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER