Simba kuja kivingine dhidi ya Yanga

Kocha Msaidizi Seleman Matola ameweka wazi kuwa mchezo wa watani wa jadi kesho dhidi ya Yanga tutaingia kivingine na kutoruhusu makosa kama kwenye michezo iliyopita ili kupata ushindi.

Kocha huyo ameongeza kuwa katika michezo kadhaa iliyopita tuliyokutana na watani wetu wamekuwa wakituponyoka lakini safari hii hatutawaruhusu kufanya hivyo.

Matola amesema maandalizi tuliyofanya kuelekea mchezo wa kesho ni makubwa na wachezaji wapo katika hali nzuri na kila mmoja yupo tayari kwa mechi.

“Hakuna Derby rahisi siku zote, tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka Yanga lakini sisi tumejiandaa kushinda na malengo yetu ni kutetea ubingwa wa Ligi tukiwa na michezo mkononi,” amesema Matola.

Wakati huo huo, Matola amesema licha ya kuwa utakuwa mchezo wa Derby lakini tumejipanga kuonyesha soka safi la kuvutia na sio kubutua butua.

“Hata kama ni Derby tumejipanga kuonyesha soka safi la kueleweka, hatutaki kubutua butua tunataka kutoa burudani kwa mashabiki,” amesema Matola.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER