Simba kuitumia Gwambina kama ngazi ya kurejea kileleni

Timu yetu leo itashuka dimbani kuikabili Gwambina FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania kwenye Uwanja wa Gwambina uliopo Misungwi na endapo tutashinda tutapaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Tangu kuanza kwa msimu huu hatujapata nafasi ya kukalia usukani wa ligi na leo kama tutaibuka na ushindi tutakaa kwenye nafasi yetu tuliyoizoea.

Hadi sasa tuko nafasi ya pili kwenye msimamo tukiwa na pointi 55 alama mbili nyuma ya wanaoongoza ambapo leo tukishinda tutakuwa juu yao kwa alama moja.

Kocha Mkuu, Didier Gomez amekiri mchezo utakuwa mgumu kutokana wapinzani wetu Gwambina kutoka kupoteza mechi mbili mfululizo za ugenini hivyo leo wasingependa kukosa pointi nyumbani.

Kocha Gomez amesema amewaandaa wachezaji kimwili na kiakili kuelekea mchezo wa leo na kila mmoja yuko tayari na uhakika wa kushinda mchezo ni mkubwa.

TAARIFA YA KIKOSI

Katika mchezo wa leo tutakosa huduma ya wachezaji wanne ambao ni Taddeo Lwanga, Pascal Wawa, Luis Miquissone sababu ya kadi tatu za njano huku Perfect Chikwende akikosekana pia.

MECHI YA MWISHO TULIPOKUTANA

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Septemba 26 mwaka jana tuliibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Mabao hayo yaliwekwa kambani na washambuliaji Medie Kagere, Chris Mugalu na mlinzi wa kati Pascal Wawa.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

  1. Katika uwanja Mgumu naamini approach ya mwalimu itaendana na kikosi atakachopanga leo,Kila la heri mabingwa,tuanze Safari ya kupigwa na baridi pale kileleni

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER