Simba kuingia kambini leo kuivutia kasi Jwaneng Galaxy

Kikosi chetu kitaingia kambini baada ya mazoezi ya leo jioni tayari kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Mchezo huo utapigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumapili saa 10 jioni ambapo tiketi zinaendelea kuuzwa kupitia mitandao ya simu ambapo viingilio vimeshatangazwa.

Baada ya kikosi kurejea kutoka nchini Botswana kilipopata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza, wachezaji walipewa mapumziko mafupi kabla ya kurejea mazoezini.

Wachezaji wawili tu mshambuliaji akiwamo Chris Mugalu na kiungo Pape Sakho hawatakuwa sehemu ya kikosi kitachoingia kambini kutokana na kuendelea kuuguza majeraha.

Katika mchezo huo tunahitaji ushindi au sare aina yoyote na kama ikitokea tumepoteza iwe bao moja na hapo tutakuwa rasmi tumeingia hatua ya makundi ya michuano hiyo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER