Simba kuingia kambini kujiandaa na Red Arrows

Kikosi chetu kitaingia kambini leo baada ya mazoezi ya jioni kujiandaa na mchezo wa kwanza wa mtoano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows kutoka Zambia.

Mchezo wetu wa kwanza dhidi ya Arrows utafanyika Novemba 28, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam saa 10 jioni.

Tunakutana na Arrows tukiwa na morali kubwa chini ya Kocha Pablo Franco ambaye ametuwezesha kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 kwenye mchezo wetu uliopita wa Kigi Kuu ya NBC dhidi ya Ruvu Shooting.

Baada ya matengenezo katika eneo la kuchezea (pitch) kukamilika kikosi kimerejea kufanya mazoezi katika Viwanja yetu vya Mo Simba Arena vilivyopo Bunju.

Tangu kuanza kwa msimu timu imekuwa ikifanya mazoezi katika Uwanja wa Boko Veterans kupisha matengenezo hayo ambayo tayari yamekamilika na kikosi kimerejea rasmi nyumbani.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER